You are currently viewing KLONS MELODY AFUNGUKA KUTOFAIDI NA MAPATO NYIMBO ZAKE SALDIDO

KLONS MELODY AFUNGUKA KUTOFAIDI NA MAPATO NYIMBO ZAKE SALDIDO

Aliyekuwa msanii wa Saldido International Klones Melody amefunguka tusiyoyajua kuhusu muziki wake akiwa chini ya lebo hiyo.

Katika mahijiano na Presenter Ali, Klones amesema hajawahi pata mapato ya nyimbo zake zote alizofanya akiwa chini lebo ya saldido international i ayomilikiwa na Willy Paul.

Amesema licha ya kumueleza Willy Paul kuhusu suala la miraba ya nyimbo zake bosi huyo hakuwahi taka kuweka wazi namna atakavyofaidi na mapato ya nyimbo alizofanya akiwa chini lebo hiyo kwani alianza kumchezea mchezo wa paka na panya.

Hata hivyo ameenda mbali zaidi na kudai kuwa Willy Paul alimuondoa studio kwake kwa njia ya mabavu akiwa kwenye harakati za kuiandaa EP yake mpya jambo ambalo lilimkasirisha kiasa cha kufanya kuigura lebo hiyo.

Hata hivyo amesema licha kwamba aliondoka kwenye lebo hiyo bila idhini yao mawakili wake wapo mbioni kuhakikisha anavunja kabisa mkataba wake wa miaka 5 na Saldido ila awe msanii wa kujitegemea.

Utakumbuka Klones Melody alijiunga na saldido mwaka wa 2017 ambapo alisaini mkataba wa miaka mitano na lebo hiyo lakini alijiondoa miezi minne iliyopita baada ya kutofautia kimawazo na uongozi wa Saldido.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke