You are currently viewing KLONS MELODY AFUNGUKA MANYANYASO ALIYOYAPITIA CHINI SALDIDO INTERNATIONAL

KLONS MELODY AFUNGUKA MANYANYASO ALIYOYAPITIA CHINI SALDIDO INTERNATIONAL

Aliyekuwa msanii wa Willy Paul, Klons Melody amefunguka sababu zilizompelekea kujiondoa kwenye lebo ya muziki ya saldido international mwishoni mwa mwaka wa 2021.

Katika mahojiano na Nicholas Kioko msanii huyo Willy Paul alikwenda kinyume na mkataba waliotia saini naye kipindi anajiunga na lebo hiyo, hivyo ikawa kizingiti kwake kufanikisha ndoto zake za kuupeleka muziki wake kwenye kiwango kingine.

Klons Melody ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao BIMA amedai kwamba alipokuwa chini ya saldido Willy Paul alibana sana asijihusishe na masuala ya muziki kwani mara nyingi alijipata anafanya usafi na kupika chai jambo ambalo anadai lilimpa msukumo wa kuondoka Saldido.

Hata hivyo amesema licha ya kwamba alipitia manyanyaso kwa mikono ya Willy Paul ataendelea kumpa heshima kwa kuwa alimshika mkono na kumtambulisha kwenye tasnia ya muziki hadi mashabiki wakamfahamu.

Utakumbuka Klons Melody alijiunga na lebo ya Saldido inayomilikiwa na Willy Paul mwaka wa 2017, na chini lebo hiyo alifanikiwa kushirikishwa kwenye nyimbo mbili ambazo ni Odi Love, na Atoti Jaber.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke