You are currently viewing Kocha Atto Oddo akosoa mwamuzi wa mechi ya Ghana dhidi ya Ureno

Kocha Atto Oddo akosoa mwamuzi wa mechi ya Ghana dhidi ya Ureno

Kocha wa Ghana Atto Oddo amemkosa mwamuzi kwa kutoa adhabu ya mkwaju wa penati ambayo imempa nafasi Cristiano Ronaldo kuweka rekodi ya magoli katika mchuano wa Kombe la Dunia kwa kuiita hatua hiyo kama zawadi maalumu.

Ushindi wa jana kwa Ronaldo unamfanya awe mchezaji pekee wa kwanza wa kiume kuibuka na ushindi katika michuano mitano tofauti ya Kombe la Dunia.

Katika mechi hiyo Ureno Ureno iliibuka na ushindi wa magoli 3-2 mbele ya Ghana.

Kocha Addo amesikika akisema ” kama mtu amefunga goli anastahili pongezi. Lakini goli hili kwa kweli ilikuwa zawadi maalum. Sina zaidi la kusema, ilikuwa ni zawadi maalum kutoka kwa kocha.”

Ukosoaji huo wa moja kwa moja wa Addo kwa mwamuzi Ismail Elfath unaweza kumwingiza matatizoni na Shirikisho la Kandanda ulimwenguni FIFA.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke