Kocha wa Klabu ya Tusker Robert Matano amedai kwamba hatamzuia nyota wa timu ya taifa Harambee Stars Boniface Muchiri kuondoka klabuni humo.
Matano amesema ameumizwa na kitendo cha mchezaji wake Boniface kucheza mechi yake ya mwisho kwenye klabu hiyo ikizingatiwa alikuwa kiungo muhimu kwenye klabu ya Tusker FC.
Hata hivyo Matano amekiri kwamba haijakuwa jambo rahisi kwake kukubali mchezaji huyo kuondoka kwenye klabu ya Tuskers kutokana na ubora wake.
Muchiri amekuwa sehemu ya wana Tusker FC tangu mwaka 2017, lakini ameamua kujiunga na Ulinzi Stars inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uliunzi Stars.
Disemba 12 mwaka huu Boniface Muchiri aliichezea klabu yake ya Tusker FC kwenye mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Sofa Paka, mechi ambayo ilitoka sare ya kutofunga katika uga wa Ruaraka Grounds Jiji Nairobi,.