Rapa kutoka nchini Marekani Kodak Black amemuomba Hakimu ruhusa ya kutoka nje ya Mji Atokao wa Florida wakati huu yupo chini ya uchunguzi.
Kulingana na taarifa za kuaminika zilizotolewa na Tovuti Ya Tmz, Muuguzi wa karibu wa Kodak anaamini rapa huyo atafaidika na ratiba ya matibabu atakayopatiwa nje ya Florida katika siku zake 30 za mwisho za kupata matibabu nje ya mji huo.
Hata hivyo timu nzima ya Kodak Black wanafikiria kwamba rapa huyo atafanikiwa zaidi na matibabu iwapo atakuwa katika mazingira tofauti kwa muda fulani.
Ombi hilo limekuja siku chache tu mara baada ya Kodak Black ku-tweet na kuwashtua mashabiki zake kwamba huenda akawa na matatizo ya akili kwani aliandika kwamba ana huzuni, na anajiona mpweke kabla ya kuzifunga kurasa zake za mtandao wa Twitter & Instagram.