Rapa Kodak Black kutoka Marekani ametaka rais wa zamani wa Marekani Donald Trump arejeshwa mamlakani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram rapa huyo ameandika ujumbe unaosomeka “Bring Trump Back” akiashairia Kwamba Ameukumbuka Utawala Wa Rais Donald Trump
Kodak Black Aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais Trump, Januari 20 mwaka huu Ambapo ilikuwa siku ya mwisho kwa Rais Huyo kukaa Ikulu ya Marekani
Kodak Alitumikia kifungo kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa kosa la kugushi nyaraka za Serikali kujipatia silaha. Kodak alifungwa miezi 46 gerezani na kifungo chake kilikuwa kimalizike 2022.