Rapa kutoka nchini Marekani, Kodak Black amesema mwaka 2022 anataka kuiondoa laana ya kwenda jela tofauti na miaka mingine.
Kodak Black amesema tangu atimize miaka 14 hajawahi kumaliza mwaka bila kwenda jela na kwa sasa anataka abadili historia hiyo.
Kodak Black ameongeza kwa kusema kwa sasa ameshaachana na mwenendo mbaya wa maisha na nguvu zake zote sasa atazielekeza kwenye muziki.
Utakumbuka Kodak Black alikuwa miongoni mwa wafungwa waliopatiwa msamaha na aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump, mwaka wa 2021. Rapa huyo alikuwa akitumikia kifungo cha miezi 46 gerezani kwa makosa ya kugushi nyaraka za Serikali kujipatia silaha.