You are currently viewing KOEMAN ATIMULIWA BARCELONA

KOEMAN ATIMULIWA BARCELONA

Hatimaye kocha Ronald Koeman amefutwa kazi ya kuendelea kukitumikia kikosi cha FC Barcelona baada ya kuwa usukani kwa miezi 14 pekee.

Barca imevuna alama 15 pekee katika mechi 10 za La Liga msimu huu, ambapo tayari wamepoteza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Koeman anafukuzwa akiwa kwenye nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi alama sita pungufu ya kinara Sevilla baada ya kupokea kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Rayo Vallecano siku wa kuamkia Oktoba 28. Kipigo kikiwa cha tatu kwa Barcelona katika mechi nne zilizopita kikifuatiwa na kile cha mtani wake Real Madrid mtanange wa El Clasico.

Taarifa rasmi ya klabu imesema kuwa “Rais wa klabu (Joan Laporta) amempa taarifa ya kufutwa kazi muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi dhidi ya Rayo Vallecano”.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke