You are currently viewing KOFFI OLOMIDE AFUTIWA MASHTAKA YA KUWASHAMBULIA KIGONO DANCERS WAKE.

KOFFI OLOMIDE AFUTIWA MASHTAKA YA KUWASHAMBULIA KIGONO DANCERS WAKE.

Mahakama ya rufaa nchini Ufaransa imemuondolea Koffi Olomide mashtaka ya kuwashambulia kingono dancers wake wanne, lakini imemhukumu kwa kuwashikilia pasipo ridhaa yao.

Mahakama hiyo ya huko Versailles, haijamkuta Koffie na hatia ya ubakaji ambapo jaji amedai kuwa ushahidi wa walalamikaji ulikuwa unakinzana na wenye kubadilikabadilika.

Hata hivyo imemhukumu kwa kuwanyima uhuru dancers hao kwa kuwaweka kwenye nyumba kuanzia mwaka 2002 hadi 2006.
Dancers hao walidaiwa kufungiwa kwenye chumba na kusimamiwa na watu wawili wa Koffi Olomide muda wote na huku mapazia yakiwa yamefungwa.

Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba, amekuhumiwa miezi 18 ambayo hata hivyo hatokwenda jela (suspended sentence) na kuwalipa fidia kwani ameamriwa awalipe kila mmoja faini ya kuanzia shilingi milioni 1.3 hadi milioni 4.1za Kenya

Mahakama hiyo imeitengua hukumu ya mwaka 2019 iliyomkuta na hatia staa huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ya kumbaka dancer wake wa kike aliyekuwa na miaka 15.

Mwendesha mashtaka wa serikali alitaka muimbaji huyo ahukumiwe kifungo cha miaka minane. Mwanasheria aliyekuwa akiwawakilisha watatu kati ya wanawake hao amesema hukumu hiyo lazima itakuwa imewaangush

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke