You are currently viewing KONSHENS AMTOLEA UVIVU ERIC OMONDI

KONSHENS AMTOLEA UVIVU ERIC OMONDI

Kufuatia mjadala ambao anauendeleza mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi akipaza sauti juu ya wasanii wa Kenya kutotendewa haki na waandaaji wa matamasha ya muziki, staa wa muziki wa dancehall Konshens ameamua kuuvunja ukimya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Konshens ameonekana kusikitisha na maneno makali ambayo Omondi amekuwa akitoa kwa wasanii wa kigeni kwa kusema kwamba mchekeshaji huyo ana machungu na ubaguzi kwa wasanii wa nje.

Hitmaker huyo wa “Pull Up” amesema sio kwamba wasanii nje wana njaa ya  pesa ila ni upendo wa mashabiki wao ndio imechangia pakubwa wao kuja Kenya kufanya shows Kenya.

Konshens ambaye atarajiwa kufanya shoo kenya kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka ameahidi kuwa akitua kenya atatenga muda wake wakutane na Eric omondi ili asikilize lalama zake kwa kina.

Hata hivyo Eric Omondi amesisitiza kuwa sio kwamba anawapiga vita wasanii wa kigeni ila ana jaribu kuipigania tasnia ya muziki ili iweze kukubalika nchini.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke