Msanii wa muziki wa dancehall nchini KRG The Don amefungua shauri la talaka mahakamani dhidi ya mke wake Linah Wanjiru, shauri hilo limefunguliwa katika Mahakama ya Milimani Jijini Nairobi.
KRG ameweka wazi hilo kupitia instagram page yake baada ya kupost nyaraka za kisheria kuhusiana na mchakato wa talaka na kusindikiza na caption inayosomeka “kwa wale waliyokuwa wanachukulia kwa mzaha, poleni”
Hitmaker huyo Giddem alifunga ndoa na mke wake huyo mwaka wa 2014 na wamejaliwa kupata wawili kwa pamoja.
Hatua ya KRG kufungua shauri la talaka dhidi mke wake inakuja siku chache baada ya kumsuta vikali mke wake huyo kwa madai ya kujihusisha sana na anasa na kusahau kuwahudumia watoto wao.