You are currently viewing KRG THE DON AFUNGUKA CHANZO CHA KUACHANA NA MKE WAKE.

KRG THE DON AFUNGUKA CHANZO CHA KUACHANA NA MKE WAKE.

Mwanamuziki wa dancehall nchini Krg The Don amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya tuhuma za kutalikiana na mke wake.

Kulingana na Krg waliachana na mke wake kwa sababu kuna baadhi ya watu ambao waliingilia ndoa yao na kumfanya mke wake huyo kuingia na kiburi.

Mwanamuziki huyo ambaye amekuwa akijinasibu kuwa ni tajiri amesema baada ya kuachana na mke wake huyo hakuchukua gari aina Audi Q7  aliyomzawadi kwenye birthday yake kama jinsi ambavyo watu wanavyodhani.

Ikumbukwe wiki iliyopita Krg The Don alidaiwa kufungua shauri la talaka mahakamani dhidi ya mke wake Linah Wanjiru.

Bosi huyo wa Cash group Entertainment alifunga ndoa na mke wake huyo mwaka wa 2014 na wamejaliwa kupata wawili kwa pamoja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke