You are currently viewing KRG The Don afunguka kustaafu muziki

KRG The Don afunguka kustaafu muziki

Msanii Krg The Don amedai kuwa hana mpango wa kustaafu muziki hivi karibuni hadi pale tasnia ya muziki nchini Kenya itazalisha takriban mabilionea 10.

Kwenye mahojiano na SPM Buzz amesema wasanii wa Kenya wana uwezo mkubwa wa kuwa matajiri ila wanapaswa kutia bidii zaidi kwenye kazi zao ikiwemo kuwekeza katika suala la kutoa nyimbo zenye ubora.

KRG The Don ambaye amekuwa akijinasibu kuwa billionea upande wa tasnia ya muziki nchini amesema kama rapa mkongwe kutoka Marekani Jay Z aliweza kufanikisha mchakato wa kuzalisha mabillionea kama Rihanna na Kanye West, haoni kitu kitakachomzuia kutengeneza mazingira ya wasanii wa Kenya kuingiza kipato kupitia muziki wao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke