Msanii KRG The Don ameweka wazi kiasi cha pesa ambacho anatumia kuwalipia watoto wake karo kwenye shule moja ya kifahari jijini Nairobi.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha radio nchini KRG amesema huwa anatumia shillingi millioni 4.8 karo ya watoto wake kwa mwaka.
Hitmaker huyo wa “Wano” amesema mtoto wake wa kwanza huwa analipa shillingi laki 7, wapili laki 6 huku watatu akiwa analipa laki 3.
KRG ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa kati ya shillingi billioni 6 na 8 za kenya amedokeza kuwa mtoto wake mwingine yupo mbioni kujiunga na shule ambapo ameahidi kuweka wazi karo yake ambayo ametaja itakuwa maelfu ya fedha.