Mwanamuziki kutoka Kenya KRG The Don amedai kwamba yeye ndiye aliifuta akaunti mpya ya instagram ya mwanablogu mwenye utata nchini humo Edgar Obare.
Kupitia instagram page yake KRG ameandika ujumbe wa kejeli kwenda kwa wafuasi wa Edgar Obare kwa kusema kwamba alikuwa ametishia kuifuta akaunti ya mwanablogu huyo ya Instagram ila watu walichukulia kama mzaha.
“I had said i will delete BNNKE for this planet they though I was joking” ..alisema KRG The Don kupitia Instagram yake.
Hata hivyo wafuasi wa KRG The Don wameonekana kutofauti kimawazo na msanii huyo kwa kusema kwamba wanamjua aliyedukua akaunti ya Instagram ya Edgar Obare.
Utakumbuka KRG The Don aliingia kwenye ugomvi na Edgar Obare baada ya mwanablogu huyo kuchapisha taarifa akihoji kuwa utajiri wa mwanamuziki huyo umetokana na biashara ya ulanguzi wa pesa ambayo amekuwa akifanya kwa muda.
Akaunti ya kwanza ya Instagram ya Edgar Obare ilifutwa mara baada ya mwanablogu huyo kuwa kero kwa mastaa mbali mbali nchini kwa kuanika maovu yao yote kupitia ukurasa wake huo.
Jaribio lake la kuirejesha akaunti yake ya kwanza ya Instagram iligonga mwamba na ndipo akafungua akaunti nyingine ambayo juzi kati ilidukuliwa na mtu asiyejulikana ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahoji kuwa ni mchekeshaji Jalang’o ndiye alidua akaunti hiyo kwani hajakuwa na maelewano mazuri na Edgar Obare.