You are currently viewing KRG THE DON AKANUSHA TUHUMA ZA KUFANYA BIASHARA YA ULANGUZI WA PESA

KRG THE DON AKANUSHA TUHUMA ZA KUFANYA BIASHARA YA ULANGUZI WA PESA

Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo kutoka Kenya KRG The Don amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa anajihusisha na biashara ya ulanguzi wa pesa bandia (Wash Wash).

Akipiga stori na Mpasho hitmaker huyo wa “Wano” amesema madai hayo hayana ukweli wowote bali yaliibuliwa na watu wanaomuonea wivu kutokana na mafanikio ambayo ameyapata akiwa na umri mdogo.

Bosi huyo wa Cash Group Entertainment amesema anamiliki biashara mbali mbali ambazo zinamuingizia kipato ambacho kinafadhili maisha yake ya kifahari.

Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa utajiri wake wa sasa umechangiwa pakubwa na hatua ya yeye kuwakimbia marafiki wabaya ambao kipindi cha nyuma alikuwa anatumia nao pesa kiholela kwa kujihusisha na vitendo vya anasa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke