You are currently viewing KRG THE DON AONYESHA JEURI YA PESA ZAKE

KRG THE DON AONYESHA JEURI YA PESA ZAKE

Mwanamuziki wa dancehall nchini Krg The Don ameamua kutuonyesha jeuri ya pesa zake baada ya kutoa zawadi ya shilllingi laki 6 kwa kundi la Mbuzi Gang.

Hitmaker huyo “Giddem” ametumia ukurasa wake wa instagram kujinasibu kwa kupost video akihesabu shillingi laki sita za Kenya ambazo amezitaja kuwa ni zawadi kwa wasaniii wa kundi la Mbuzi Gang ambao kwa mujibu wake walishirikiana nae na vizuri kwenye mchakato wa kuandaa nyimbo zake ambazo ni “Mchecheto” na “Densi.”

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameonekana kutofautiana kimawazo na Krg The Don wakisema msanii huyo anatumia pesa hizo kama kiki ya kuupromote nyimbo zake mpya.

Ikumbukwe mapema wiki hii Krg The Don alifungua shauri la talaka mahakamani dhidi ya mke wake Linah Wanjiru, ambaye juzi kati alimsuta vikali kwa madai ya kujihusisha sana na anasa na kusahau kuwahudumia watoto wao.

Bosi huyo wa Cash Group Entertainment alifunga ndoa na mke wake huyo mwaka wa 2014 na wamejaliwa kupata wawili kwa pamoja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke