Walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamemshambulia mwanamuziki wa dancehall nchini KRG The Don mara baada ya msanii huyo kuomba ushauri awanie kiti gani cha kisiasa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Kupitia instagram page yake KRG The Don alidai kuwa amekuwa akipokea shinikizo kutoka kwa marafiki zake wa karibu kujiunga na siasa.
Sasa kupitia uwanja wa comment wa post yake mashabiki wamemtolea uvivu Krg The Don wakisema kuwa hapaswi kuwania kiti chochote cha kisiasa kwani hana kabisa vigezo vya kuwa kiongozi.
Haikushia hapo wameenda mbali zaidi na kumshauri KRG The Don aendelee kufanya muziki wa Gengetone huku wengine wakidai kuwa msanii huyo anajaribu kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye media ikizingatiwa kuwa muziki umemshinda.