Baada ya uvumi wa wiki kadhaa, Msanii wa muziki wa Dancehall nchini KRG The Don hatimaye amethibitisha kuwa yeye na mke wake sio wapenzi tena.
KRG ameweka wazi hilo kupitia Instagram page yake baada ya kupost picha ya mke wake huyo na kusindikiza na caption inayoashiria kuwa wameachana rasmi.
Hitmaker huyo “Giddem” amemsuta vikali mke wake huyo kwa madai ya kujihusisha sana na anasa na kusahau kuwahudumia watoto wao.
KRG pia ametumia fursa hiyo kukanusha madai yanayosambaa kwenye mitandao kuwa alitoka nje ya ndoa yake na ndio maana uhusiano wake na Baby mama wake ulivunjika.
Hata hivyo, bado haijabainika kama kuna ukweli wowote kuhusu stori za wawili hao kuachana ila kwa sasa wamefuta picha zote walizowahi kupiga wakiwa pamoja kwenye mtandao wa Instagram.