You are currently viewing KRG THE DON AWAJIA JUU VIJANA WANAOTUMIA SHENG NCHINI KENYA

KRG THE DON AWAJIA JUU VIJANA WANAOTUMIA SHENG NCHINI KENYA

Mwanamuziki KRG the Don amewatolea uvivu vijana wanaotumia lugha ya Sheng yenye maneno yasiyoeleweka nchini Kenya.

Kulingana na KRG, kundi la vijana wanaotumia lugha hiyo ni malimbukeni ambao wana fikra za kikoloni.

“Hiyo ni ujinga, hiyo ni primitivity of the highest order! …iko sheng ile poa… You are going backwards !… ata kama mtu alikua anataka kukuambia anakupenda umuambie nakulombotov, si anaenda kama stima…,” Krg amesema kwa masikitiko.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ushasema” amewataka vijana wajifunze mambo yatakayowasaidia maishani badala ya kutumia lugha isiyokuwa na mashiko kwenye jamii.

“Hizo vitu vijana wametoka sijui wamevuta gum…wanaamka wanaanza kuongea vitu sasa ata ukiulizwa hizo vitu…itawasaidia nini?  Utatoka na hiyo vitu uende utafute kazi gani ? Mi naoana hiyo ni kama kurudi reverse kwa Maisha. Kwa sababu badala ujue lugha yenye unaeza kuongea, Ata si afadhali ujifunze kiChinese… Ukiongea Kichenese, sa hizi watu karibu 1. Something billion wananongea Kichenese, unaeza enda ata china ukafanya kazi ,sasa ukianza kuongea vitu yenye ni wewe na beshtee yako munaelewa,”…Amesema KRG

Kauli yake imekuja mara baada ya msanii Jeshi Jinga na Madocho kuingia kwenye bifu ya ni nani hasa ndiye muasisi wa lugha bora ya sheng nchini Kenya.

Sheng ni lugha legevu isiyozingatia kanuni za kisarufi ambayo mara nyingi huzungumzwa na vijana wengi nchini Kenya kwa kuchanganya Kiswahili na Kingereza pamoja na lugha za ndani vile Kikuyu,Kijaluo na nyingine nyingi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke