You are currently viewing KRG THE DON AWATOLEA UVIVU WASANII WA MBOGI GENJE KWA KUDAI WIMBO WA ZIBLE NI WAO

KRG THE DON AWATOLEA UVIVU WASANII WA MBOGI GENJE KWA KUDAI WIMBO WA ZIBLE NI WAO

Mwanamuziki wa dancehall nchini KRG The Don amenyosha maelezo kuhusu umiliki wa wimbo wa Zible aliowashirisha wasanii wa kundi la Mbogi Genje baada ya kundi hilo kudai kuwa KRG aliiba ubunifu wao.

Katika mahojiano yake hivi karibuni KRG The Don amesema wasanii wa Mbogi Genje hawakugharamia chochote kwenye mchakato wa kuandaa wimbo huo, hivyo hawana haki ya kudai mirabaha ya wimbo wa Zible.

KRG The Don amewatolea uvivu wasanii wa Mbogi Genje kwa kutumia lugha isiyokuwa na mashiko kuwasilisha ujumbe kwa mashabiki, kitu ambacho amedai kuwa imekuwa kizingiti kwa muziki wao kusikilizwa na watu wa umri wote katika jamii.

Hitmaker huyo wa “Full kishunzi” amepuzilia mbali madai ya wasanii wa Mbogi Genje kuwa walimuandikia wimbo wa zible kwa kusema kwamba madai hayo hayana msingi wowote kwani alihusika pakubwa kuandika wimbo huo bila usaidizi wa mtu yeyote.

Kauli ya KRG The Don imekuja mara baada ya wasanii wa kundi la mbogi genje kumtuhumu kuwa alishindwa kuwalipa alipowashirikisha kwenye wimbo wake uitwao Zible ambapo walienda mbali zaidi na kusema kwamba wao ndio walihusika kwa asilimia moja kwenye uandishi wa wimbo huo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke