You are currently viewing KRG THE DON AWEKA WAZI THAMANI YA UTAJIRI WAKE

KRG THE DON AWEKA WAZI THAMANI YA UTAJIRI WAKE

Msanii asiyeishiwa na vituko kila leo Krg the Don amejigamba kuwa ana utajiri wa kima cha kati ya shillingi billioni 6 na 8 za Kenya.

Katika mahojiano yake bosi huyo Cash Group Entertainment amesema katika kipindi cha miaka kumi ijayo thamani ya mali yake itakuwa imeongezeka hadi shillingi trillioni moja za Kenya kwani anazidi kuwekeza kwenye nyanja mbali mbali itakakayomuingizia kipato zaidi.

KRG ambaye anafanya vizuri na singo yake mpya “Wano” amesema mafanikio makubwa ambayo ameyapata akiwa na umri mdogo ndio yamewafanya baadhi ya watu kuanza kumchukia na hata kumzushia tuhuma za uongo mitandaoni, jambo ambalo amedai alitamkatisha tamaa kwenye suala la kujitafutia riziki na kuishi maisha yake ya kifahari.

Utakumbuka katika siku za hivi karibuni utajiri wa msanii huyo umekuwa ukitiliwa shaka huku wengi wakihoji kwamba huenda chanzo cha utajiri wake umetokana na yeye kushiriki kwenye biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya madai ambayo amekuwa akipuzilia mbali.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke