Rapa The Game kutoka Marekani amekasirika sana baada ya kukosa nafasi ya kutumbuiza kwenye Halftime show ya Super Bowl 2022, Wiki iliyopita alitokwa mapovu na kusema 50 Cent hakustahili kupewa nafasi hiyo.
Meneja wake aitwaye Wack 100 ameibuka na kutusanua makubwa ambayo hatuyafahamu nyuma ya pazia. Wack 100 amesema The Game alimtukana Jay-Z tusi zito “Suck My D**k” baada ya kumnyima nafasi ya kutumbuiza kwenye Halftime show ya fainali hizo za mwaka huu.
Utakumbuka Roc Nation ya Jay Z waliingia makubaliano na NFL kuwa waandaaji wa burudani kwenye Super Bowl 2022.
Kinyongo baina ya wasanii hao kilianza mwaka 2005 baada ya The Game kudai kwamba alijibiwa vibaya na Jay-Z walipokutana kwenye mgahawa wa 40/40 mjini New York ambapo The Game alimuomba ushauri Jigga ya namna ya kudumu muda mrefu kwenye muziki.