Wasanii wa kundi la B2C Boys wamemtolea uvivu Bebe Cool kwa kuiponda wimbo wao uitwao “It’s Okay” ambao wameimba kwa mtindo wa amapiano.
Wasanii hao wamemtaka Bebe Cool kukoma kuingilia mambo yao na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye suala la kuboresha muziki wake.
“Hawezi kufikiria kwa ajili yetu. Njia yake ya kufanya mambo sio sawa na yetu. Hatuwezi tu kupata pesa kupitia harusi. Tulifanya amapiano kulenga soko la kimataifa na tumefaidika,” watatu hao walieleza.
Ikumbukwe Bebe Cool alisema kuwa kundi la B2C wanaua brand zao na kupoteza rasilimali kwa kufanya mtindo huo wa muziki. Alienda mbali zaidi na kusema kuwa hawatapewa nafasi ya kutumbuiza wimbo huo kwenye sherehe za harusi kutokana na ubovu wa wimbo huo.