Kundi la muziki kutoka nchini Korea Black Pink wameweka rekodi mpya kwenye mtandao wa youtube.
Black pink wamekuwa wasanii wenye Subscribers wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwani wamefikisha Subscribers MILIONI 70.
Kundi hilo linaundwa na wasichana wanne; Jisoo, Jennie, Rosé, na Lisa.
Chaneli yao ya youtube ilifunguliwa rasmi Juni 29 mwaka 2016 ambapo ndio waliachia album yao wa kwanza iitwayo Square One na mpaka sasa chaneli hiyo ina jumla ya views Bilioni 21.3