Members wa kundi maarufu la muziki duniani BTS maarufu kama Bangtan Boys kutoka Korean kusini kwa pamoja wanatarajiwa kujiunga na jeshi la nchi yao kupata mafunzo katika kipindi cha miezi 18 kama katiba na sheria ya nchi yao inavyo sema.
Kundi hilo maarufu duniani linaloundwa na wanamuziki 7′ kwa pamoja wanatarajiwa kupata mafunzo hayo ndani ya mwaka huu 2022 ambayo ni ya lazima kwa kijana yoyote mwenye umri kati ya miaka 18 mpaka 27 aneyeishi korea kusini.
Utakumbuka mwaka 2020 mchezaji nyota wa klabu ya Tottenham Hotspur ya ligi kuu nchini Uingereza Son Heungmin aliweza kushiriki mafunzo hayo na kupatiwa cheti na tuzo maalumu kuhitimu mafunzo.