Kundi maarufu la Muziki toka Korea Kusini – BTS limetangaza kupumzika kufanya kazi kama Kundi hadi mwaka 2025.
Kundi hilo liliundwa mwaka 2010 na kuanza kufanya vizuri mwaka 2013 ambapo katika kipindi hicho wamefanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwemo kushinda Tuzo kubwa mbali mbali na kutawala chart kubwa za Muziki duniani.
Sababu ya kufikia maamuzi hayo ni kutaka kila mmoja afanye kazi binafsi (solo projects) lakini pia sababu nyingine kubwa ni kutimiza takwa la Kisheria ambapo baadhi ya memba watajiunga na mafunzo ya Kijeshi kwa mujibu wa sheria za nchi yao kuanzia Oktoba mwaka huu.