Kundi maarufu la muziki kutoka Korea la BTS, limetangaza rasmi kuchukua mapumziko ya kazi kwa sasa kama kundi huku likieleza kila memba wa kundi hilo atafanya muziki kivyake.
Kwenye taarifa yao kupitia channel yao ya youtube wameeleza watarudi baadae na kisha kuendelea na kazi za pamoja.
Kundi hilo lenye mafanikio makubwa, linaloundwa na wasanii 7 ambao wamekuwa pamoja kwa takribani miaka tisa linaongozwa na RM, Jung Kook, V, Jimin, Suga, Jin na J-Hope.
“Tutarudi upya na kufanya makubwa zaidi” – ameeleza Jung Kook.
Hata hivyo hii inakuwa mara ya tatu kwa kundi hilo kutangaza kuchukua mapumziko, mara ya mwisho kutangaza hivyo ilikuwa ni mwaka 2019 na kisha baadae kurejea kwa kishindo.