You are currently viewing KUNDI LA MASAKA KIDS KUTOKA UGANDA LATAJWA KUWANIA TUZO ZA NICKELODEON KIDS CHOICE 2022

KUNDI LA MASAKA KIDS KUTOKA UGANDA LATAJWA KUWANIA TUZO ZA NICKELODEON KIDS CHOICE 2022

Kampuni ya Nickelodeon imeweka orodha ya majina ya watu walioteuliwa kuwania tuzo za Nickelodeon Kids Choice Awards mwaka 2022.

Goods ni kwamba kwa upande wa Afrika Mashariki tunawakilishwa na Kundi la kucheza muziki kutoka nchini Uganda Masaka kids Africa ambao wamechaguliwa kuwania tuzo hizo mwaka huu kupitia kipengele cha Favourite African Kid Influencer ambapo watachuana na Adaeze Onuigbo wa Nigeria,  Sassy Taylor Morrison, Uncle Vinny, and Witney Ramabulana wote kutoka Afrika Kusini.

Orodha ya washiriki wa kuwania tuzo za Nickelodeon Kids Choice Awards  mwaka 2022 imewekwa wazi na kampuni hiyo kupitia tovuti yao ambapo tayari watu wameanza kupiga kura kupitia tovuti hiyo hiyo KidsChoiceAwards.com

Tuzo hizo zitatolewa ifikapo Aprili 13, na zoezi zima litaonyeshwa katika channel za runinga ya waandaji wa tuzo hizo pamoja na programu ya matangazo ya moja kwa moja katika vifaa vya iPad, iPhone, na Android kwa wakazi wa nchini Marekani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke