You are currently viewing KUNDI LA MBOGI GENJE LATHIBITISHA KUWA KIBIASHARA ZAIDI BAADA YA KUANIKA MKEKA UNAONESHA BEI YA KUFANYA COLLABO NA SHOWS

KUNDI LA MBOGI GENJE LATHIBITISHA KUWA KIBIASHARA ZAIDI BAADA YA KUANIKA MKEKA UNAONESHA BEI YA KUFANYA COLLABO NA SHOWS

Kundi la muziki wa Gengetone nchini Mbogi Genje limetangaza kuwa kibiashara zaidi mara baada ya kuanika mkeka Unaonesha kiwango cha pesa wanachotoza kwa watu wanaotaka kufanya nao kazi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mbogi genje wamesema kwamba kwa kila msanii anayetaka kufanya kolabo nao atalazimika kuwalipa shillingi laki 3 za Kenya huku wakiwataka waandaji wa matamasha kuwalipa shillingi elfu 150 kwa ajili ya kuwashirikisha kwenye shows zao.

Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kuwapongeza kwa hatua ya kugeuza muziki wao kuwa biashara zaidi huku wengine wakionekana kuwabeza kwa kulipisha pesa nyingi kwa shows na kolabo wakati muziki wao hauna mashiko

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke