You are currently viewing KUNDI LA MUZIKI WA GENGETONE, BOONDOCKS GANG LAVUNJIKA RASMI

KUNDI LA MUZIKI WA GENGETONE, BOONDOCKS GANG LAVUNJIKA RASMI

Msanii wa kundi la Boondocks Gang, Madoxx amethibitisha rasmi kuvunjika kwa kundi hilo ambalo lilikuwa linaundwa na wasanii Exray na Odi wa Muranga.

Katika Mahojiano yake ya hivi karibuni na Presenter Ali, Madoxx amesema wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo Exray na Odi walianza kumtelekeza kwa kumu-unfollow kwenye mtandao wa Instagram mara baada ya kuachia wimbo wao wa mwisho uitwao Dhidhi miezi 6 iliyopita .

Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba amekuwa akipitia manyanyaso kwenye suala la ufanyaji kazi katika kundi la Boondocks kwani kwa kipindi cha muda mrefu amekuwa akipewa verse za mwisho kwenye nyimbo zao ambazo wamekuwa wakiziachia.

Maddox amedai kuwa uongozi wa Boondocks umekuwa na upendeleo kwa wasanii Exray na Odi wa Murang’a kwa kuwa walipewa ruhusa ya kufungua chaneli zao za mtandao wa youtube huku wakimbania kufungua chaneli yake binafsi ili aweze kuachia nyimbo zake kama msanii wa kujitegemea.

Hata hivyo amesema hana ugomvi wowote na wasanii wenzake Exray na Odi wa Murang’a huku akikanusha kupata usaidizi kutoka kwa uongozi wa Boondocks baada ya taarifa yake kusambaa mtandaoni kuwa amefungiwa nyumba aliyokuwa akiishi kutokana na kushindwa kulipa kodi.

Utakumbuka kundi la Boondocks Gang lilikuwa linaundwa na wasanii watatu Exray, Odi wa Murang’a na Maddox na lilipata umaarufu nchini mwaka wa 2019 kupitia muziki wenye mahadhi ya Gengetone.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke