Msanii mkongwe wa Bongofleva, Lady Jaydee ametangaza ujio wa album yake mpya iitwayo “Love Sentence” ambayo amemshirikisha msanii mwenzake Rama Dee.
Jide amesema, album yao ina jumla ya nyimbo 10 zote zikiwa za mapenzi ambapo amefichua kuwa nyimbo 2 ambazo ni Matozo na I Found Love tayari zimeshatoka.
Uzinduzi wa album hiyo utafanyika Februari 10, mwaka 2023 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.