Msanii mkongwe kwenye muziki nchini uganda Lady Mariam amepuzilia mbali madai ya kuchukua mapumziko kwenye muziki wake.
Hitmaker huyo wa “Tindatine” amesema bado anajishughulisha na masuala ya uimbaji ila kwa sasa anahitaji mtu ambaye atawekeza kwenye muziki wake kwa kuwa muziki umebadilika pakubwa.
“Sijawahi kuacha muziki kama watu wengi wanavyodhani. Bado naimba lakini nahitaji mtu wa kuwekeza katika taaluma yangu kwa sababu muziki umebadilika sana,” alieleza katika mahojiano.
Lady Mariam ambaye ana kiu ya kurudi kwenye game ya muziki Afrika Mashariki, juzi kati alitoa rai kwa mapromota wamzingatie kwenye shows zao kwani bado ana uwezo wa kutoa burudani kwa mashabiki.