Msanii kutoka nchini Uganda Lady Mariam anayejulikana sana na wimbo wake maarufu uitwao “Tindatine” amerudi tena kwenye headlines.
Msanii huyo anatuhumiwa na dadake mkubwa, Kirungi Swabra kwa kukimbia na pesa zake alizozichuma kwa bidii. Swabra ambaye anafanya kazi kama mjakazi katika miliki za Kiarabu alitaka kutumia pesa hizo kununua nyumba huko Mityana nchini Uganda.
Kulingana na swabra alimtumia lady mariam shillingi laki 2 za Kenya aongeze na mkopo wa shillingi 6 ambao angechukua kwa niaba yake kununua nyumba yenye thamana ya shillingi laki 8 lakini msanii huyo hakufuata maagizo aliyompa.
Swabra, ameenda mbali zaidi na kudai kwamba Mariam anajihusisha na vitendo vya kishirikina kama njia ya kujikwamua kiuchumi.
Lady Mariam, hata hivyo, ameibuka na kudai kwamba hamfahamu Swabra kwani anatumia jina lake kujitafutia umaarufu.