Msanii anayekuja kwa kasi nchini Larota ameachia rasmi Album yake mpya aliyoipa jina la Dala.
Album hiyo ambayo ameitaja kuwa inaeleza ndoto anayotamani kutimiza kwenye muziki wake, imebeba jumla ya mikwaju 11 ya moto huku ikiwa na kolabo 2 kutoka Iddi Singer na Melo Banjo.
Dala Album ni kazi ya kwanza kutoka kwa Larota tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kusikiliza na kuuza muziki duniani.