You are currently viewing Lebron James aendelea kumuenzi Take Off

Lebron James aendelea kumuenzi Take Off

Nyota wa mpira wa kikapu ulimwenguni Lebron James maarufu kama King James ameendelea kumuenzi aliyekuwa rapa kutoka kundi la Migos, Take Off aliyefariki Novemba 1 mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram King James ameandika “Kama unanifahamu basi unajua kiasi gani nilimpenda Take Off, kwangu bado siamini kama ni kweli hatupo naye!”

Nyota huyo wa kikapu siku ya jana alivaa nguo za mfanano na nguo alizowahi kuvaa rapa Take Off, ikiwa ni katika kuendelea kumuenzi rapa huyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke