Mwanamuziki kutoka uganda Leila Kayondo na bwenyenye SK Mbuga walikuwa wapenzi mwaka wa 2012 hadi 2015 walipovunja mahusiano baada ya kuingia kwenye ugomvi mkali.
Leila alimtuhumu SK kwa kumnyanyasa kijinsia kwa kumshushia kipigo kila mara na akaamua kumuacha kabisa.
Lakini cha kushangaza amejitokeza sasa na kudai kwamba hakuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na bwenyenye huyo ikizingatiwa kuwa walikuwa wanafurahia maisha pamoja.
“Sijawahi chumbiana na Sk Mbuga. Tulikuwa tu tunafurahia maisha.”,Alisema kwenye mahojiano na runinga ya NBS .
Hata hivyo SK Mbuga hajatoa kauli yoyote kuhusu madai yaliyoibuliwa na msanii huyo ikizingatiwa kipindi cha nyuma jamaa huyo alimzawadi gari aina BMW kama njia ya kumuonyesha mapenzi.