Lengo la Jay-Z kujiunga na mtandao wa instagram limefahamika. Deina Kirk, mwanamke ambaye anahusika na masuala ya masoko katika kampuni ya Netflix, amesema alimshauri Jay-Z ajiunge na mtandao huo kwa masaa 24 kwa ajili tu ya kuitangaza filamu yake mpya “The Harder They Fall” ambayo amehusika kama mtayarishaji.
Baada ya kutikisa vichwa vya habari kwa siku nzima Novemba 4 mwaka huu Jay-Z aliwashtua wengi kwa kuifuta akaunti yake ya Instagram ikiwa na zaidi ya followers milioni 2 na kitiki cha blue.
Mkongwe huyo wa Hip Hop na mfanyabiashara alikuwa sio muumini wa mitandao ya kijamii kabisa, aliwahi kukaririwa akisema; Mitandao ya Kijamii ni mahususi kwa wale ambao hawawezi kujieleza kwenye ulimwengu wa kawaida yaani waoga. Lakini pia ni dunia ya watu ‘feki’ ambao watakuchukia bila sababu kutokana na ukweli kwamba wana mapenzi zaidi kwenye mtindo huu wa maisha kuliko hata binadamu wenzao.
Tovuti ya Billboard inaarifu kwamba Jay-Z aliwahi kujiunga na mtandao wa Instagram Agosti 29 mwaka wa 2015 na kumtakia heri ya kuzaliwa marehemu Michael Jackson lakini aliifuta akaunti hiyo ndani ya masaa 14 akiwa tayari amevuna followers laki moja.