You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 30, ALIZALIWA STAA WA MUZIKI KUTOKA NCHINI ENGLAND,DES’REE

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 30, ALIZALIWA STAA WA MUZIKI KUTOKA NCHINI ENGLAND,DES’REE

Siku kama ya leo Novemba 30 mwaka wa 1968 alizaliwa Staa wa muziki wa RnB na pop kutoka Uingereza, Des’ree.

Jina lake halisi ni Desire Annette Weekes na alizaliwa huko London nchini England ambako alianza muziki mwaka wa 1991 alipoachiwa single yake iitwayo” Feel So High” chini ya lebo ya muziki Sony 550.

Mwaka wa 1992 Desree aliachia album yake ya kwanza iitwayo “Mind Adventures” ambayo ilikuwa na jumla ya ngoma 10 ikiwemo Feel So High, Average Man na nyingine kibao.

Mwaka wa 1994 Desree aliachia album yake ya pili iitwayo “I Aint Movin”, album hiyo ya jumla ya ngoma ilifanikiwa kuuza zaidi ya nakala millioni 2.5 kote duniani.

Mafanikio ya album yake ya  “I Aint movin” ilimpelekea kupata   ziara ya kimuziki nchini Marekani mwaka wa 1995 akiwa na msaani mwenzake kutoka England aitwaye Seal.

Mwaka wa 1996 wimbo wake uitwao “Kissing you” ilitumika kama soundtrack ya filamu ya William Shakespeares iitwayo Romeo and Juliet.

Mwaka wa 1998 wimbo wake ulipokelewa kwa uzuri kwenye nchini nyingi zilizopo Barani Ulaya na kumpelekea Desree kupata tuzo ya Brit Award kupitia kipengele cha msaani bora wa kike wa kujitegemea.

Mwaka wa 2000 Desree aliachia album iliyokuwa ibeba nyimbo zilizotaka na zile hazikutoka  iitwayo “Endangered Species” ikafuatwa na album iitwayo “Dream Soldier” ya mwaka wa 2003 ambayo ilikuwa na jumla ya singles 12.

Mwaka wa 2003 desree alichukua mafupi kwenye muziki baada ya lebo ya muziki ya Sonny 550 kuvunja mkataba wake lakini mwaka wa 2019 aliacha album yake iitwayo “A love story” baada ukimya wa miaka kumi na sita kwenye muziki chini ya lebo ya muziki ya Stargazer.

Hata hivyo tangu aanze muziki mwaka wa 1991 Desree ameshafanya jumla ya tano za muziki na ameshateuliwa kwenye tuzo mbali mbali ambapo ameshinda tuzo ya Brit Awards,World music Awards, na nyingine kibao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke