Siku kama ya leo Novemba 10 mwaka wa 1978 alizaliwa mwiigizaji na rapa wa kike kutoka Marekani, Eve.
Jina lake halisi Eve Jihan Jeffers na alizaliwa huko Philadelphia, Pennsylvania nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 1996 akiwa na kundi la Dope Girl Posse lakini baada ya kundi hilo kuvunjika alihamua kufanya muziki wake kama msaani wa kujitegemea.
Mwaka wa 1998 akiwa chini ya lebo ya muziki ya aftermath inayomilikiwa na rapa mkongwe kutoka marekani Dr. Dre, Eve alishirikishwa kwenye kazi kadhaa za wasaani wa lebo hiyo lakini mwaka wa 1999 aliachia album yake ya kwanza iitwayo “Let Be There Be Eve…Ruff Ryders First Lady.
Album hiyo iliyotayarishwa na lebo ya muziki Ruff Rryders Entertainment kwa ushirikiano na lebo ya Interscope Records ilifanikiwa kufikia viwango vya mauzo ya Platinum mara mbili kwa kuuza zaidi ya nakala millioni 2.
Baada ya album yake ya kwanza kufanya vizuri sokoni mwaka wa 2001 Eve aliachia album yake ya pili iitwayo “Scorpion”, album ambayo ilitoa ngoma kama “Let Me Blow Your Mind” na “No Doubt” ambazo zilishika namba mbili kwenye chati ya billboard hot 100.
Mwaka wa 2002 Eve aliachia album yake ya tatu iitwayo “Eve-olution”,album ambayo ilifanikiwa kufikia viwango vya Gold, kwani iliweza kuuza zaidi ya nakala laki 5 nchini Marekani pekee.
Mwaka wa 2007 alitangaza ujio wa album yake ya nne iitwayo “Lip Lock” lakini kutoelewana na lebo ya muziki ya Interscope alihamua kubadilisha jina na kuita “Am To Flirt” na baada ya kuigura lebo ya InterScope mwaka wa 2012 eve alihamua kuiachia album hiyo ya “Lip Lock” binafsi.
Hata hivyo tangu aanze muziki mwaka wa 1996, Eve ameshafanya jumla ya album 4 za muziki, singles 32, na video 29 za muziki.
Kutokana na mafaniko aliyoyapata kwenye muziki, Eve ametauliwa kushiriki kwenye tuzo mbali mbali za muziki nchini Marekani na ameshinda tuzo ya Grammy, tuzo 2 za BET, MTV music Awards na nyingine kibao.