You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 12, ALIZALIWA NYOTA WA MUZIKI WA RNB KUTOKA MAREKANI, OMARION.

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 12, ALIZALIWA NYOTA WA MUZIKI WA RNB KUTOKA MAREKANI, OMARION.

Siku kama ya leo Novemba 12 mwaka wa 1984 alizaliwa Staa wa muziki wa RnB na HipHop kutoka nchini Marekani, Omarion.

Jina lake halisi ni Omari Ishmael Grandyberry na alizaliwa huko Carlifonia nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 1998 akiwa na kundi la B2K.

Mwaka wa 1999 Omario akiwa na kundi la B2K waliachia single yao ya kwanza iitwayo “Uh Uh” ikafuatwa na album yao ya kwanza iitwayo  “B2K” ya mwaka 2002. Baada ya album hiyo kufanya vizuri sokoni mwaka huo kundi la “B2K” liliachia album ya pili iitwayo “Pandemonium”

Mwaka wa 2004 baada ya kundi la “B2K” kuvunjika Omarion alianza kufanya muziki kama msaani wa kujitegemea ambapo mwaka wa 2005 aliachia ya album ya kwanza inayokwenda kwa jina la O.

Baada ya album ya O kushika na namba moja kwenye chati ya BillBoard Hot 200 Omarion aliachia album yake ya pili iitwayo “21” mwaka wa 2006, album ambayo ilifikia viwango vya mauzo vya Gold kwa kuuza zaidi  ya nakala 39000 nchini Marekani  pekee..

Mwaka wa 2007 Omarion pamoja na rapa mkongwe kutoka Marekani Bow Bow walirekodi album ya pamoja iitwayo “Face off”, album ambayo iliweza kufikia viwango vya Gold kwani iliweza kuuza zaidi ya nakala laki 5.

Mwaka wa 2009 Omarion alisaini mkataba wa kufanya kazi na lebo ya muziki ya Young Money Entertainment lakini miezi 4 baada aliigura lebo hiyo na kuzindua lebo yake iitwayo “StarrWorld Entertainment”  ambapo aliachia singles mbili ikiwemo  “I Get It In” na “Speedin”.

Mwaka wa 2011 Omarion aliachia Mixtape yake iitwayo “The Awakening”  lakini mwaka wa 2012 alisaini mkataba na lebo ya muziki ya Roc Nation ambapo aliachia EP mbili kwa mpigo ambazo ni “Care Package” na “Care Package 2” ambazo zilitoka mwaka wa 2013.

Hata hivyo tangu aanze muziki mwaka wa 1998, Omarion ameshafanya jumla ya album 5 za muziki, EP 2, mixtape moja, singles 30 na ameshirikiishwa na wasaani wengine kwenye album 3 za muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke