You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 13, ALIZALIWA ALIYEKUWA NGULI WA MUZIKI WA RUMBA KUTOKA CONGO TABU LEY ROCHEREAU
Tabu Ley Rochereau performing at a 2003 festival in Hertme, Netherlands.

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 13, ALIZALIWA ALIYEKUWA NGULI WA MUZIKI WA RUMBA KUTOKA CONGO TABU LEY ROCHEREAU

Siku kama ya leo Novemba 13 mwaka wa 1937 alizaliwa aliyekuwa mwanazumiki tajika wa Rumba kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, Tabu ley Rochereau.

Jina lake halisi ni Pascal Emmanuel Sinamoyi Tabu, na alizaliwa huko Bandundu Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ambako alianza maisha yake ya muziki mwaka wa 1959 akiwa na kundi maarufu la African Jazz lililokuwa chini ya Joseph ‘Grande Kalle’ Kasebele,

Tabuley alikuwa mmoja wapo wa walioimba ule wimbo utunzi wa Grande Kalle, na uliotikisa anga la Afrika miaka ya 60, Independence Cha Cha, uliogeuka na kuwa wimbo rasmi wa kusherehekea uhuru wa Congo.

Baada ya miaka minne, Tabuley aliigura bendi ya African Jazz  na kujiunga na bendi ya African Fiesta waliyounda na mpiga gitaa mahiri nchini Congo Nicholaus Kassanda, lakini mwaka wa 1965, Tabuley, aliaachana na Dr. Nico na kuanzisha bendi yake binafsi iitwayo African Fiesta,, wanamuziki kama Papa Wemba na Sam Mangwana ni kati ya wakongwe waliowahi kupitia katika bendi hiyo.

Mwaka wa 1970, Tabu ley alianzisha bendi ya Orchestre Afrisa International, wakati huo Afrisa na TPOK Jazz ndizo zilikuwa bendi maarufu zaidi Afrika. Afrisa waliachia vibao kama Sorozo, Kaful Mayay, Aon aon, na Mose Konzo ambazo zilimpelekea Tabu ley kupata tuzo kutoka serikali za nchi kama Chad iliyompa heshima ya Officer of the National Order, wakati Senegal ilimpa heshima ya Knight of Senegal, na akawa sasa anaitwa Siegneur Rochereau.

Katikati ya miaka ya 80 Tabu ley aligundua kipaji cha mwanamama aliyekuja kutikisa anga za Afrika naye si mwingine bali ni mwanamama Mbilia Bel, baadae Tabuley alimuoa Mbilia na wakapata mtoto mmoja aitwaye Melodie lakini mwaka wa 1988 Tabu ley alimgundua muimbaji wa kike mwingine aitwaye Faya Tess jambo ambalo lilimfanya Mbilia Bel kuigura bendi ya Afrisa International na kuendelea na maisha yake ya muziki kama msaani wa kujitegemea.

Kipindi hiki, mtindo wa Soukous uliokuwa na mapigo yenye mwendokasi zaidi ya lile Rumba la Afrisa na TPOK Jazz ulianza kuzishika nyoyo za vijana, bendi hizi kubwa zikaanza kufifia.

Baada ya album yake ya “Trop, Cc’est Trop kupigwa marufuku na serikali ya Mobutu Sseko mwanzoni mwa miaka ya 90, Tabu ley alihamia nchini Marekani na kuishi kusini mwa California, ambapo alibadili muziki wake katika kujaribu kujikita zaidi katika soko la ‘kimataifa’, akatunga nyimbo kama Muzina, Exil ley, Babeti Soukous.

Mwaka wa 1997 baada ya serikali ya Mobutu kuondolewa mamlakani, Tabu ley alirejea nchini kwao Congo  ambapo alipewa cheo cha uwaziri katika utawala wa rais Laurent Kabila, hata baada ya kifo cha Laurent Kabila Novemba mwaka wa 2005 Tabu ley alipewa cheo cha unaibu gavana, kwenye jiji la Kinshasa.

Mwaka 2006 Tabu ley akashirikiana na rafiki yake wa muda mrefu Maika Munah na kutoa album yake ya mwisho iliyoitwa Tempelo, katika album hiyo kuna wimbo ambao ni kama kumbukumbu ya kote alikopita na pia akaimba wimbo mmoja na binti yake Melodie.

Mwaka 2008 alipata mshtuko wa moyo na hakika kuanzia hapo hali yake haikurejea kawaida hadi kifo kilipomchukua siku ya Jumamosi Novemba 30 mwaka wa 2013 akiwa na umri wa miaka 73, katika hospital ya St. Luc Bsusells  nchini Ubelgiji.

Tabuley” katika kazi yake ya muziki hadi kufariki dunia, aliacha album 250 za muziki, nyimbo 3000 alizorekdi na watoto 104.

Laiti kama Tabuley  angelikuwa hai Novemba 13 mwaka wa 2021, tungelisherehekea miaka 84 ya kuzaliwa kwake lakini kwa masikitiko makubwa, siku hii ndugu na wapenzi wa muziki wa mzuri wa Rumba wanaomboleza miaka 8 tangu kifo chake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke