You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 14, ULIMWENGU HUADHIMISHA SIKU YA KISUKARI DUNIANI.

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 14, ULIMWENGU HUADHIMISHA SIKU YA KISUKARI DUNIANI.

Siku kama ya leo Novemba 14 kila mwaka ulimwengu huadhimisha  Siku ya Kisukari Duniani kwa lengo la kuongeza mapambano na kubadilishana uzoefu baina ya wadau.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani za mwaka 2015 zinakadiria kuwa watu milioni 415 wanaugua ugonjwa huu, idadi hii inatarajiwa kufikia milioni 642 ifikapo mwaka 2040 kama hatua za kukabiliana nao hazitochukuliwa.Tayari idadi imeongezeka mpaka milioni 422 mwaka huu.

Inaelezwa kwamba ifikapo mwaka 2040, kutakuwa na wagonjwa milioni 642. Afrika kulikuwa na wagonjwa milioni 14.2 wa kisukari mwaka 2015 na idadi hii inakadiriwa kuongezeka hadi kufikia watu milioni 34.2.

Ni wajibu wa kila mwanajamii kuyafahamu mambo kadhaa kuhusu ugonjwa huu ambao unashika kasi katika nchi zenye uchumi mdogo na wa kati zikiwamo nyingi za Afrika.  Kwa Kenya, ugonjwa huo unaendelea kukua kwa kasi hali inayotishia maendeleo endelevu ya ustawi wa uchumi wa nchi

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke