You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 15, ALIZALIWA ALIYEKUWA RAIS WA KENYA, MWAI KIBAKI

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 15, ALIZALIWA ALIYEKUWA RAIS WA KENYA, MWAI KIBAKI

Siku kama ya leo  Novemba, 15 mwaka wa 1931 alizaliwa aliyekuwa rais wa tatu wa Kenya Emilio Mwai Kibaki katika eneo bunge la Othaya, Kaunti ya Nyeri.

Safari ya kisiasa ya Bwana Kibaki ilianza mwaka wa 1963 alipochaguliwa kama mbunge wa Doonholm jijini Nairobi kupitia chama cha KANU. Eneo bunge hilo lilibadilishwa jina na kuitwa Bahati miaka ya 60 na tena likapewa jina jipya la Makadara ambalo bado linatumika hadi leo.

Alichaguliwa kwa mara nyingine kama Mbunge wa Bahati kwenye uchaguzi wa mwaka wa 1969 na akahudumu hadi 1974 alipoitikia wito wa wakazi wa Othaya wa kumtaka awanie uchaguzi wa mwaka huo katika eneobunge lake la nyumbani.

Ndoto ya Bwana Kibaki ilitimia Disemba mwaka wa 2002 aliposhinda urais kwa asilimia 62 za kura baada ya kuungwa mkono na viongozi wa upinzani pamoja na waasi wa chama cha KANU.

Alichaguliwa kukamilisha hatamu yake ya uongozi mwaka wa 2007 kwenye uchaguzi tata uliopingwa vikali na mpinzani wake Raila Odinga aliyedai aliibiwa ushindi.

Katika muda wa miaka 50 alizoshirikia siasa za nchi, Bwana Kibaki ametajwa na wengi kama kiongozi mnyamavu ambaye msimamo wake kuhusu masuala kadhaa ya kitaifa haujitokezi waziwazi kwa urahisi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke