You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 17, ALIZALIWA ALIYEKUWA MWANASOKA WA URENO NA KLABU YA MANCHESTER UNITED, LUIS NANI.

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 17, ALIZALIWA ALIYEKUWA MWANASOKA WA URENO NA KLABU YA MANCHESTER UNITED, LUIS NANI.

Siku kama ya leo Novemba 17  mwaka wa 1986 alizaliwa mwanasoka wa zamani wa Ureno na klabu ya Manchester, Luis Nani.

Jina lake halisi ni Luis Carlos Almeida da Cunha na alizaliwa huko Amadora nchini Ureno ambako alianza soka katika timu ya vijana ya Sporting CP kabla ajejiunga na klabu kubwa ya Sporting CP ya nchini Ureno.

Akiwa Sporting CP Nani aliweza kusaidia klabu hiyo kutwaa kombe la klabu bingwa nchini Ureno maarufu kama Taca de Portugal ambapo aliichezea klabu hiyo mechi 58 huku akifunga magoli 9 kwa misimu miwili aliyoitumikia klabu ya Sporting Lisbon.

Mwaka wa 2007 nani alitimukia nchini England na kuidaka saini ya klabu ya Manchester United kwa pauni millioni 25 ambapo aliisaidia klabu hiyo mataji manne ya Premier,matano ya Ngao ya Jamii,kombe la klabu Bingwa la FIFA duniani na taji la klabu bingwa barani Ulaya. Kwa misimu saba aliyoitumikia klabu ya Manchester Nani aliichezea klabu hiyo mechi 147 huku akifunga magoli 25.

Mwaka wa 2015 klabu ya Manchenster United ilimtuma nani kwenda kuitumikia klabu yake ya zamani ya Sporting Lisbon kwa mkopo kwa msimu mmoja kabla ya kuuzwa kwenda kutumikia klabu ya Fenerbanche  kwa pauni millioni 4.25.

Akiwa Fenerbanche  Nani alifanikiwa kuichezea klabu hiyo mechi 29 huku akitia kimiani magoli 8 kwa msimu mmoja. Kando na Fernebahce, Nani amezitumikia klabu za Valencia,Lazio na Orlando city.

Katika ngazi ya Kitaifa, Nani ameichezea timu ya taifa ya soka ya Ureno mechi 112 huku akifunga magoli 24  tangu mwaka wa 2006 kwenye mashindano mbali mbali aliyoitumikia taifa lake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke