You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 23,ALIZALIWA STAA WA MUZIKI WA POP DUNIANI, MILEY CYRUS

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 23,ALIZALIWA STAA WA MUZIKI WA POP DUNIANI, MILEY CYRUS

Siku kama ya leo Novemba 23 mwaka wa 1992  alizaliwa staa wa muziki  wa Pop na Hiphop kutoka nchini Marekani, Miley Cyrus.

Jina lake halisi ni Destiny Hope Cyrus na alizaliwa huko Franklin Tennesse nchini Marekani ambako alianza kama muigizaji wa kipindi cha runinga cha Hannah Montana kabla ya kuanza muziki mwaka wa 2007 alipoachia album yake ya kwanza iitwayo  “Meet Miley Cyrus”.

Album hiyo ilifanikiwa kushika namba mbili kwenye chati ya Billboard 200  na kuuza zaidi ya nakala milllioni 3 nchini Marekani. Mwaka wa 2008 Miley Cyrus aliachia album yake ya pili iitwayo “Breakout” ikafuatwa na EP yake ya kwanza iitwayo “The Times of our Lives” ya mwaka wa 2009.

Mwaka wa 2010 Miley Cyrus aliachia album yake ya tatu iitwayo “Can’t Be Tamed,album ambayo haikufanya vizuri sokoni kwani ilikuwa album yake ya kwanza  kushindwa kushika namba moja kwenye chati ya Billboard 200.

Mwaka wa 2013 Miley Cyrus alijiunga na lebo ya muziki ya RCA Records ambapo aliachia album yake ya nne iitwayo “The Banger”,ambayo ilifanya vizuri sokoni kwa kushika namba moja kwenye chati ya Billboard 200 huku ikiuza nakala 270,000 ndani ya wiki tangu iichiwe rasmi.

Mwaka wa 2015 Miley Cyrus aliachia album yake ya tano iitwayo “Miley Cyrus & Her Dead Petz” ikafuatwa na album ya sita iiitwayo “Younger now” iliyotoka mwaka wa 2017.

Hata hivyo tangu aanze muziki mwaka wa 2007  Miley Cryus ameshafanya jumla ya album 6 za muziki,EP 4,Soundtrack 5, na singles 33.

Kando na muziki, Miley Cyrus ameshiriki kwenye vipindi vya runinga na filamu mbali mbali nchini Marekani ikiwemo Big Fish ya mwaka wa 2003,Bolt ya mwaka wa 2008,Lol ya mwaka wa 2012 na nyingine kibao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke