Siku kama ya leo novemba 4 mwaka wa 1969 alizaliwa staa wa muziki wa Hiphop kutoka Marekani, P. Diddy.
Jina lake halisi ni Sean John Combs na alizaliwa huko Mount Vermon jijini New York, nchini Marekani ambako alianza kujihusisha na masuala ya muziki alipokuwa chini ya mwavuli wa Uptown Reconds klabu ya kuanzisha lebo yake ya Bad Boy Entertainment mnamo mwaka wa 1993.
Mwaka 1997 P.Diddy aliachoa albamu yake ya kwanza iitwayo “No Way Out”, album ambayo ilifanikiwa kufikia viwango vya mauzo ya Platinum mara saba.
Albamu nyingine zilizofanikiwa sana sokoni kutoka kwa P. Diddy ni “Forever” ya mwaka wa 1999, “The Saga Continues” ya 2001 na “Press Play” ya mwaka wa 2006.
Mwaka wa 2009 P. Diddy aliunda kundi la muziki wa Hiphop liitwalo “Dirty Money” ambapo lilifanikiwa kuachia album yao ya kwanza mwaka wa 2010 inayokwenda kwa jina la “Last Train to Paris”.
Hata hivyo tangu aanze muziki mwaka wa 1993 P. Diddy ameshafanya jumla ya album saba za muziki, album moja ya iliyobeba ngoma alizofanyia remix, Singles 72 ikiwemo 33 ambazo alifanya kama msaani wa kujitegemea na 39 alizoshirikishwa na wasaani wengine.
Kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye muziki wake, P. Diddy ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo mbali mbali za muziki nchini marekani na ameshinda tuzo tatu za Grammy tatu na mbili za MTV lakini, pia tuzo katika usanifu wa fasheni.
Jarida la Forbes mwaka wa 2018 lilitaja utajiri wake kufikia dola milioni 825 lakini pia amekuwa na skendo nyingi tu ikiwemo kifo cha Rapa mahiri wa West Coast Tupac Amar Shakur.
Miaka 15 baada ya kifo cha West Coast rapper Tupac Shakur, mpelelezi wa zamani wa LAPD, Greg Kading alimtaja Sean ‘Diddy’ Combs kwenye kitabu chake cha Murder Rap, kuwa alihusika na alifadhili mauaji ya Rapa Tupac Shakur. Kitabu cha mpelelezi huyo kilitoka Oktoba 4, mwaka wa 2011 na kilijumuisha ushahidi wa kutosha kutoka kwa kaseti na kumbukumbu kutoka kwa watu muhimu waliohojiwa kuhusiana na mauaji ya 2Pac.