Siku kama ya leo Oktoba 13 mwaka wa 1980 alizaliwa staa wa muziki wa RnB na Hihop kutoka nchini Marekani Ashanti.
Jina lake halisi ni Ashanti Shequoiya Douglas na alizaliwa huko Glen Cove, New York nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 2001 kipaji chake kilipotambuliwa na prodyuza mkali kutoka marekan Irv Gotti ambaye alimshirikisha kwenye wimbo uitwao Whats Luv wake Fat Joe na always on time wa Jah Rule.
Kutokana na uwezo ambao alionyesha kwenye collabo hizo Ashanti alisaini mkataba wa kufanya kazi na lebo ya muziki Murder Inc ambayo ilisimamia kazi zote za album yake ya kwanza iitwayo Eponymous ya mwaka wa 2002,album ambayo iliweza kufikia viwango vya mauzo ya Platinum kwa kuuza zaidi ya nakala milllioni 6 nchini Marekani.
Mwaka wa 2003 ashantia aliachia album yake ya pili iiitwayo Chapter II ambayo ilifanikiwa kushika namba moja kwenye chati ya billboard 200 lakini pia ikafanikiwa kufikia viwango vya mauzo ya platinum kwa kuuza nakala millioni 1.5.
Mwaka huo huo Ashantia aliachia ya tatu iiitwayo Christmas ikafuatwa na Concrete Rose ya 2004, Declaration ya mwaka wa 2008 na Braveheart ya 2014 album ambazo hazikufanya vizuri kwenye soko la muziki ikilinganishwa na album zake za awali.
Hata hivyo mpaka sasa ashanti ameshafanya jumla album 6 za muziki, singles 24, na video 21 za muziki wake akiwa chini lebo ya muziki Murder Inc,Def Jam na Motown.
Kutokana na mafanikio ambayo aliyapata kwenye muziki wake nchini Marekani Ashanti ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo 89 za muziki na ameshinda tuzo 35 ikiwemo 8 za Billboard Music Awards, 3 za American Music,moja ya Grammy na nyinngine kibao.
Kando na muziki, Ashanti ni muigizaji ana ameshiriki kwenye filamu nyingini nchini marekani ikiwemo Coach Carter,John Tucker Must Die na nyingine kibao.