You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MKALI WA RnB KUTOKA MAREKANI USHER

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MKALI WA RnB KUTOKA MAREKANI USHER

Siku kama ya leo Oktoba 14 mwaka wa 1978 alizaliwa Staa wa muziki RnB kutoka nchini Marekani Usher.

Jina lake halisi ni Usher Raymond IV na alizaliwa huko Dallas, Texas nchini na kukulia Atlanta, Georgia nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 1994 alipoachia album yake ya kwanza iitwayo Usher.

Lakini mwaka wa 1997 ndipo Usher alipopata umaarufu baada ya kuichia albamu yake ya pili iitwayo MY WAY,ambayo ndani yake kulikuwa na wimbo uitwao NICE & SLOW ambao ulishika namba moja kwenye Billboard hot 100.

Hakuishia hapo,albamu yake tatu ya mwaka wa 2001 iliyoitwa 8701 ilitoa wimbo ambao wengi leo tunaimfahamu kwa jina la U REMIND ME ambao nao ulishika namba moja pia kwenye Billboard hot 100.

Mwaka 2004 alitoa albamu ya nne iliyoitwa CONFESSIONS albamu iliyouza zaidi  ya nakala million 10 kwa marekani pekee na kupewa hadhi ya viwango vya mauzo ya DIAMOND,ndani yake kulikuwa na vibao vikali kama YEAH,BURN na MY BOO.

Mwaka 2008 usher alitoa albamu ya tano iitwyo HERE I STAND ndani kukiwa na hits kali kama LOVE IN THIS CLUB ambayo nayo ilishika namba moja kwenye chati ya Bllboard hot 100.

Hata hivyo mpaka sasa usher ameshafanya jumla ya album 8 za muziki, EP 8, Singles 79 na album 10 za nyimbo zilizotoka pamoja na zile hazikutoka akiwa chini ya lebo ya muziki ya La Face,Arista, Jive na RCA Records.

Kutokana na mafanikio ambayo aliyapata kwenye muziki wake nchini marekani Usher ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo mbali mbali za muziki na ameshinda tuzo 8 za Grammy, 18 za Billboard music Awards, 34 za ASCAP Awards, 9 za Soul train music na nyinngine kibao

Kando na muziki, usher ni mmiliki wa record lebo iitwayo vanity records na pia ameigiza kwenye filamu mbali mbali nchini marekani ikiwemo the Faculty ya mwaka wa 1998, Light it up ya mwaka wa 1999, Hustlers ya mwaka wa 2019 miongoni mwa nyingine kibao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke