You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MWANAMUZIKI KUTOKA MAREKANI KEYSHIA COLE.

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MWANAMUZIKI KUTOKA MAREKANI KEYSHIA COLE.

Siku kama ya leo oktoba 15 mwaka wa 1981 alizaliwa staa wa muziki wa RnB kutoka marekani Keyshia Cole.

Jina lake halisi ni Keyshia Myeshia Johson na alizaliwa huko Oakland Carlifonia nchini Marekani ambako alianza kujifunza kuimba ambapo marafiki zake walimtambulisha kwa rap mkongwe nchini marekani MC Hammer akiwa na miaka 12 tu na kutaka kuimba naye.

Keyshia baadae alijenga urafiki na 2 Pac ambaye alimwambia atamsaidia kwenye kumjenga kimuziki lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kufanya kazi na rapa huyo ambaye alikuja akafariki baada kupigwa risasi.

Akiwa na miaka 18 Keyshia Cole alihamia mjini Los Angeles  na kuanza kufanya kazi na wasanii kama D’Wayne Wiggings  wa  Tony Toni Tone na Messy Marv.

Mwaka 2002, alitambulishwa kama msaani wa lebo ya muziki ya A&M Records A&R Ron baada ya boss wa lebel hio kusikia wimbo wake wa “Love” ukiwa bado hujakamilika ila ulivyokamilika ulikuwa wimbo wa kwanza wa Keyshia Cole kuuza kopi milioni 1 nchini Marekani.

Mwaka wa 2005 Keyshia Cole aliachia album yake ya kwanza iitwayo The Way It Is  album ambayo ilifanikiwa kufikia viwango vya mauzo ya gold na platinum kwa kuuza zaidi ya nakala milllioni 1.6.

Baada ya kuachana lebo ya muziki ya A& M record alijiunga na lebo ya Geffen Records ambayo ilisimamia kazi zote za album yake ya pili   iliyotoka mwaka 2007 inayokwenda kwa jina la Just Like You.

Album hiyo ilifanikiwa kupata mapokezi mazuri nchini marekani kwani ilifanikiwa kushika namba 2 kwenye chati ya Billboard 200 lakini pia iliweza kufikia viwango vya mauzo ya platinum kwa kuuza zaidi ya nakala milllioni 1.7 nchini marekani pekee.

Mpaka sasa KeyshiaCcole ameshafanya jumla ya album saba za muziki, single 17, soundtrack album 6, na ameshirikishwa na wengine kwenye album 18 za muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke